Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene: TAKUKURU isijifungie ofisini

Simbachawene: TAKUKURU Isijifungie Ofisini Simbachawene: TAKUKURU isijifungie ofisini

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka ofisini na kwenda sehemu ambako huduma za kijamii zinatolewa kwa kuwa huko kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu kutondewa haki katika kupata huduma.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Watumishi wa Taasisi hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Amesema ni wakati sasa wa TAKUKURU kwenda kupambana na rushwa katika maeneo hayo badala ya kukaa ofisini huku wakisubiri kupewa taarifa za rushwa na watu wengine.

“Naitaka TAKUKURU ya sasa iende huko kwa wananchi wasio na sauti wanakopatiwa huduma za kijamii zikiwemo ardhi, elimu, afya na nyinginezo lakini kuna kero kubwa ya rushwa,” Mhe.Simbachawene amesisitiza.

Ameongeza kuwa chombo hiki cha TUKUKURU kinatakiwa kiende sehemu zinakotolewa huduma za kijamii na kionekane kinafanya kazi ya kusikiliza, kunusa, kutazama, kugusa na kuwabaini wale wote wanaojenga mazingira ya rushwa kwa wananchi ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Yapo maeneo mengi ambayo tumeyaona ni ya kawaida lakini yanasababisha watoa huduma wetu kuingia katika rushwa, mangúniko ni mengi juu ya rushwa, hivyo ni lazima hatua zichukulie kudhibiti hili kwa maendeleo ya taifa,” Mhe Simbachawene amesema.

Aidha, Mhe. Simbachawene amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kikamilifu, hivyo ni wakati sasa wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais kwa kufanya kazi kikamilifu katika kupamba na rushwa na kuitokomeza.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni amesema TAKUKURU imeanza kufanya kazi zake kimkakati kutoka kufanya kazi kimazoea hadi kwenye kuhakikisha wananchi wanapewa huduma za kijamii pasipo kutengenezewa mazingira ya rushwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live