Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene: Bangi bado tatizo nchini

Simba Simba Bangi Simbachawene asema bangi bado tatizo nchini

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetaja bangi kuwa bado ni tatizo sugu nchini licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

Kauli hiyo imetolea leo Juni 10, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge George Simbachawene wakati akitoa taarifa za hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2021 ambayo taarifa yake iliwasilishwa bungeni pia.

Simbachawene amesema katika kipindi hicho, tani 22.74 za bangi zilikamatwa na mamlaka hiyo ukilinganisha na tani 13.23 zilizokamatwa mwaka 2020 hivyo kuwa na ongezeko la asilimia 72 la ukamataji wa dawa hizo.

Amesema katika kipindi hicho, watuhumiwa wa biashara ya bangi 9,484 wakiwemo wanaume 8,726 walikatwa na wanawake walikuwa 758 ambalo ni ongezeko la asilimia 25 kwa watuhumiwa.

“Ongezeko la dawa na kiasi cha dawa na idadi ya watuhumiwa waliokamatwa imetokana na juhudi za mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vinginevya ulinzi na usalama na jamii kwa ujumla katika kupiga vita biashara ya dawa haramu za kulevya,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wa mirungi alisema idadi ya watuhumiwa waliokamatwa imeongezeka ukilinganisha na kipindi cha 2020 licha ya kuwa kiwango cha dawa hizo kilipungua kwa kiwango kwani 2020 walikamatwa tani 11.80 lakini 2021 walikamata tani 10.93.

Akijibu swali kuhusu wanasiasa wanaopigia chapuo bangi ihalalishwe, amesema bado kuna mjadala mrefu kuhusu jambo hilo lakini kwa sasa Serikali inafanya kazi ya kuwalinda watu wake dhidi ya dawa za kulevya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live