Mzee Said Mohamed ambaye ni Baba Mzazi wa mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amezikwa jana Jumanne, jioni katika makaburi ya kisutu Dar es Salaam.
Mzee Said alifariki dunia alfajiri ya jana Machi 01 2022 jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali na watu mashughuli pamoja na wapenzi wa Yanga, soka kwa ujumla na wafanyabiashara wamejitokea kwa wingi kumsindikiza mzee Said Mohammed katika makazi yake ya milele.
Miongoni mwao ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. 2021 - 2025. Hon. Hemed Suleiman Abdulla, naibu Spika wa Bunge, Musa Azan Zungu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na wengine wengi.
Marehemu Mzee Said alikuwa mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.
Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara na kuamua kuhamia Dar es Salaam na kuwa Wasambazaji wakubwa wa mazulia ya PVC ndani ya Tanzania na nchi jirani.
Inna lillahi wa inna ilayhi rajuun.