Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi! Mwili wa Dk. Mwele Malecela Waagwa Karimjee

Mwele Aagwa Simanzi! Mwili wa Dk. Mwele Malecela Waagwa Karimjee

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wameongoza waombolezaji viwanja vya Karimjee kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Mwele Malecela aliyefariki nchini Uswizi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mwili wa Dk. Mwele umewasili usiku wa kuamkia leo Februari 19, 2022 kutokea Geneva ambako umauti ulimkuta.



Akizungumza wakati wa kutoa salam za pole, Rais Mwinyi amesema; "Kwa muda wote ambao nimemfahamu Dkt. Mwele, kikazi alikuwa ni mtu wa kujituma sana 'committed and very professional.



"Dkt. Mwele ameitumikia Nchi yake, sisi sote tunapaswa tujiulize endapo tutaweza kufikia yale ambayo ameyafikia na ukiacha upande wa kazi kama mtu alikuwa na utu mkubwa, alikuwa karibu sana na watu alikuwa anapenda kusaidia, ameaema Mwinyi.



Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa amesema; "Nimekuja kutoa salamu za Rais

Samia Suluhu ambaye angependa kujumuika hapa kutoa pole amenituma nilete salamu za pole kwa familia kufuatia kifo cha mpendwa wetu Dkt. Mwele, amesema atakaporudi atakuja kukusalimia mzee Malecelam, amesema Majaliwa.



Baada ya kuagwa Karimjee, Mwili wa Dk. Mwele utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Dodoma kwa ajili ya maziko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live