Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silaha iliyomgusa Akwelina haijajulikana – Kamanda Mambosasa (+video)

Video Archive
Sat, 31 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema Askari Polisi waliotuhumiwa kifo cha Mwanafunzi wa chuo cha NIT, Akwina Akwiline bado uchunguzi unaendelea na haijajulikana ni silaha ipi iliyomgusa.



Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda Mambosasa amesema kuwa kama walivyotoa taarifa kutuhumiwa kwao na hata upelelezi utakapo kamilika wataeleza.

Askari waliokuwa wametuhumiwa kuhusu kifo cha Akwilina ikumbukwe kwamba walivyokamatwa tulieleze bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile. Kwahiyo bado suala la upepelezi unaendelea yapo maelekezo ambayo yaliyotolewa.Ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndiyo iliyokwenda ikamgusa Akwilina lakini askari wale kama mnavyojua walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi ni yupi alikuwa ametenda kwahiyo upepelezi bado unaendelea,“ amesema Mambosasa.

Akwelina aliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa Februari 16, 2018 wakati wa maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishinikiza Mkurugenzi wa Uchaguzi Kinondoni kutoa viapo kwa mawakala wa chama hicho.

Chanzo: bongo5.com