Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku 30 za Simbachawene kuhusu silaha

Silahaapic33 Siku 30 za Simbachawene kuhusu silaha

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene ametoa siku 30 za kusalimisha silaha haramu kwa hiari nchi nzima.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 30, 2021, Simbachawene amesema shughuli hiyo ya kusalimisha silaha itaanza Novemba Mosi hadi Novemba 30, 2021.

“Kupitia tangazo la Serikali namba 774 la Oktoba 29, mwaka huu natangaza msamaha wa kutoshtakiwa kwa wale watakaosalimisha silaha kwa hiari kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye tangazo,” amesema Simbachawene.

Amesema silaha hizo zisalimishwe katika vituo vyote vya jeshi hilo nchini na ofisi za Serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni.

Chanzo: mwananchidigital