Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule za mwendokasi marufuku

Video Archive
Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tandahimba. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amepiga marufuku maofisa elimu kusajili shule zisizokidhi vigezo kwa misukumo ya wanasiasa.

Pia, amesema hatamvumilia mkuu wa wilaya au mkurugenzi wa halmashauri ambaye wanafunzi kuna wanasomea chini ya miti.

Byakanwa alisema hayo juzi wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu.

Alisema kusajiliwa shule zisizokidhi vigezo ni chanzo cha changamoto zilizopo.

“Uhaba wa madarasa, vyoo na ofisi za walimu umetokana na udhaifu wa watendaji wetu, ilifika wakati tunasajili chumba kimoja tunaita shule, ilhali hicho chumba hakina sifa ya kuwa shule,” alisema Byakanwa na kuongeza:

“Hizi shule zinazosajiliwa kwa msukumo wa wanasiasa akija mwambie mhusika shule hiyo iwe na vigezo ili isajiliwe.”

Naye ofisa taaluma mkoani Mtwara, Felix Ndanda alisema kusajili shule ni muhimu lakini lazima kufuata vigezo vya Wizara ya Elimu vinayosimamiwa na wadhibiti ubora kanda na wilaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz