Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataja mkakati kusaidia vijana

Ma RC, DC Toeni Taarifa Za Michango Ya Wadau Kwenye Maafa   Majaliwa.jpeg Serikali yataja mkakati kusaidia vijana

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja mikakati mbalimbali ambayo tayari imeanza kutekelezwa na Serikali ili kuwatambua wabunifu, kuwasaidia kupata mitaji pamoja na kuendeleza ubunifu wao.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni Serikali kufanya mazungumzo na sekta binafsi zikiwemo taasisi za kibenki ili kufungua dirisha litakalosaidia kuwakopesha mitaji wabunifu hao.

Waziri MKuu Majaliwa ameliambia Bunge Jijini Dodoma kuwa Serikali itaendelea kuweka msisitizo na kukuza uelewa kwa wabunifu wa namna mitaji hiyo inapatikana pamoja na kuwasaidia kupata soko la kazi zao.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Buchosa,;Erick Shigongo wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu ambapo Mbunge huyo alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuanzisha Mfuko wa kuwasaidia wabunifu ili wapate mitaji na kuendeleza ubunifu wao.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huwatambua wabunifu kupitia Mfuko ulio chini ya wizara hiyo pamoja na maonesho mbalimbali ya ubunifu yanayowakutanisha kuonesha kazi zao, lakini pia imeanzisha Mifuko ya kuwasaidia wabunifu hao kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live