Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sativa aliyetekwa Dar apatikana Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya - Video

Video Archive
Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana anayetambulika kwa jina la Edgar Edson Mwakabela (27) maarufu kama Sativa mkazi wa Mbezi kwa Msuguli, Dar es Salaam ambaye alipotea tangu Jumapili, Juni 23, 2024 majira ya saa 12 jioni amepatikana amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Sativa ambaye ni mwana mtandao maarufu wa Twitter (ama mtandao wa X) alipotea saa chache baada ya kuachana na kaka yake aitwaye Patrick ambaye walikwenda naye Coco Beach kwa ajili ya kuburudisha akili.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo TZW imezipata ni kuwa, siku ya tukio Sativa alikuwa na kaka yake huyo lakini waliachana maeneo ya Ubungo wakati wanarudi.

Baada ya kaka kufika nyumbani kwake alipomwandikia ujumbe mdogo wake kutaka kujua iwapo amefika nyumbani salama, ujumbe wake haukujibiwa n ahata alipopiga simu haikupatikana mpaka usiku wa manane jambo ambalo lilimsitua na kuwajulisha ndugu ili waone namna ya kufanya.

Ndugu walifika nyumbani kwa Sativa ambapo walikuta kitasa cha mlango kimevunjwa na madirisha yakiwa wazi, walipoingia ndani hawakumkuta, jambo ambalo liliwalazimu kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Temboni ambapo waliambiwa warudi baada ya saa 24 kwa ajili ya kupewa RB.

Ndugu hawakuishia hapo, walikwenda mpaka hospitalli ya Mloganzila ili kufahamu iwapo alifikishwa hospitalini hapo akiwa mgonjwa, majeruhi au amepatwa na tatizo lolote lakini hawakumpata.

Kutokana na hali hiyo ndugu na marafiki wa Sativa walianza kupaza sauti ili waweze kupata msaada wa wanasheria, wanaharakati na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kumpata ndugu yao ambaye alikuwa amepotea na simu zake zote tatu zikiwa hazipatikani.

Post ya mwisho ya Sativa kwenye mtandao wa X ilikuwa ni kuhusu maandamano ya wafanyabiashara wa kariakoo ambapo aliposti picha ya mtu aliyepigwa mshale na kuandika “Ukikoswa na Mshale wa jicho basi kichwa lazima kiwajibike.”

Baada ya kuokotwa na wasamaria wema katika Hifadhi ya Katavi mkoani Katavi, Sativa amedai kuwa alitekwa na watu wasiojulikana ambao wamempiga na kumjeruhi vibaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live