Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia awataka wakuu wa nchi Afrika,Korea kusimamia ajenda ya nishati safi

Video Archive
Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa nchi mbalimbali duniani kuunga mkono ajenda ya Nishati Safi ya kupikia ambayo itapunguza uharibifu wa mazingira katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kiongozi huyo ametoa maoni yake kwenye Mkutano wa wakuu na Serikali kati ya Korea na Afrika unaoendelea katika mji wa Goyang, Seoul Korea, uliowaleta pamoja marais 25 na wawakilishi wa wengine 23 barani Afrika kujadili ushirikiano baina ya nchi hiyo na ukanda huo.

Amesema Nishati Safi itapunguza ukataji miti na magonjwa yatokanayo na hewa chafu na kuwaunguzia wanawake usumbufu.

"Pamoja na kuunga mkono ajenda ya Korea Afrika, na kwa kuwa mimi ndiye Rais mwanamke pekee katika chumba hiki (2024 Korea-Afrika Summit), lazima nizungumzie ajenda ambayo ni muhimu kwa mwanamke na kwa ujumla.

"Nchi yangu (Tanzania) inapenda kusisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano ili kuendeleza ajenda ya nishati safi ni sehemu yake na kuongeza uwekezaji katika suluhu za kupikia safi ambako sio tu kwamba hupunguza uzalishaji hewa chafu na kupunguza ukataji miti, lakini pia tunapunguza vifo vinavyohusiana na kupumua na kuwawezesha wanawake kufanya shughuli nyingine za kiuchumi." amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live