Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la bodaboda, bajaji kuzuiwa kuingia mjini latua bungeni

Silaaaa Sakata la bodaboda, bajaji kuzuiwa kuingia mjini latua bungeni

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Ukonga mkoani Dar es Salaam Jerry Silaa, amemuomba Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kuruhusu Bunge kujadili taarifa ya dharura kuhusu zuio la bodaboda kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Silaa amesema vijana wengi wamejiajiri kupitia shughuli hiyo hivyo kitendo cha kuzuia ni kukaribisha ukali wa maisha kwa vijana.

Hata hivyo Spika wa Bunge ametoa mwongozo kwa viongozi wanaohusika kutafuta njia mbadala na kuona namna ya kufikia muafaka, pia amegusia usafiri maarufu mkoani Kigoma 'mchomoko' kusitishwa ambapo amewashauri viongozi kutumia busara kwani usafiri huo unatumika na wananchi wengi mkoani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: