Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la binti aliyeingiliwa kinguvu na wanaume lamng'oa RPC Dodoma - VIDEO

Video Archive
Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP Camillus Wambura amemhamisha kituo cha kazi SACP George Katabazi kutoka Manyara kuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma.

Katabazi anachukua nafasi ya SACP Theopista Mallya ambaye amehamishiwa Makao Makuu.

Tukio hilo limekuja ikiwa ni baada ya Jeshi la Polisi nchini kuomba radhi kwa walioguswa na kuchukizwa na kauli ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya aliyenukuliwa na vyombo vya habari akisema “aliyedaiwa kubakwa na kulawitiwa alikuwa kama anajiuza.”

Polisi imesema kauli hiyo siyo msimamo wa Jeshi la Polisi na kwamba mwandishi aliuliza swali kuwa inadaiwa mwathirika wa tukio hilo alikuwa anajiuza, na majibu ya kamanda yalikuwa “hata kama anajiuza, hangestahili kutendewa hivyo.”

Watetezi wa haki za binadamu na utawala bora walionesha kuchukizwa na taarifa hizo na kuelezea maskitiko yao katika mitandao ya kijamii wakitaka haki kwa msichana huyo.

Msemaji wa Polisi, DCP David Misime amesema kupitia taarifa kwa umma kuwa Jeshi la Polisi litawafikisha watuhumiwa wa vitendo hivyo Mahakamani leo Agosti 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live