Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Mafuta; Mpina, Makamba Wana Chuki Binafsi? - Video

Video Archive
Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UMUAZI wa kufuta tozo ya shilingi 100 ya mafuta ungali ‘kooni’ kwa Waziri wa Nishati na Madini, January Makamba.

Shinikizo lililopo ni kwamba waziri huyo anatakiwa kujiuzulu huku Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa, akiitaka Takukuru imchunguze kwa kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 30.

Mpina katika siku za hivi karibuni amekuwa kama mchezaji anayetumia miguu yote miwili, anambana Waziri Makamba ndani ya bunge na nje kwa kuzungumzia ishu hiyo ya tozo kwa waandishi wa habari.

Waziri Makamba kwa upande wake amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni kama zinabembwa na watu wasiopenda awe waziri wa Nishati na hivyo kuleta hisia kwa baadhi ya watu kuwa huenda Mpina na yeye wana ugomvi binafsi.

Video za sakata la tozo, hoja za Makamba, Mpina na mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma zitazame kwenye video hapo juu.

Columnist: www.tanzaniaweb.live