Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la IPTL laibuka upya bungeni

Msukuma Fdr.png Joseph Kasheku 'Msukuma,' Mbunge wa Geita Vijijini

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Geita Vijiji, Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma, amehoji kwa ajili sakata la Tegeta Escrow haliishi baada ya Kampuni ya IPTL inayohusishwa na suala hilo, kuibukia mahakamani kutaka Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliipe fedha zilizotokana na utekelezaji mkataba wa kuzalisha umeme.

Msukuma amehoji hayo bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 3 Novemba 2023, akizungumzia ubadhirifu wa fedha za umma unaoripotiwa na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), bila wahusika kuchukuliwa hatua.

Mwanasiasa huyo amedai, ameanza kusikia sakata hilo kabla hajawa mbunge, lakini anashangaa hadi leo IPTL inataka ilipwe fedha.Msukuma alianza kuwa mbunge 2015 ambao anahudumu kwenye nafasi hiyo hadi sasa.

“Nataka kuzungumza kuhusu IPTL, hii IPTL toka Christopher Olesendeka alikuwa kioo change anahangaika mpaka lep. Watu wakasema hela ya mboga zikalipwa. Leo tena kizazi chetu ameibuka anataka kulipwa, ni dalili gani hizi jamani? Hizi hela zinapelekwa wapi? Kwa sababu hela ni nyingi mno zinatajwa kuibiwa mbona kwenye mabenki mzungukoni hazimo?” amehoji Msukuma.

Katika hatua nyingine, Msukuma ameitaka Serikali kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuhusika kwenye ufisadi uliotajwa katika ripoti za CAG.

Sakata la Escrow lilishika kasi 2013, ambalo liliibua mvutano bungeni juu ya uhalali wa kuchotwa fedha kiasi cha Sh. 320 bilioni, kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya TANESCO na IPTL.

Mnamo 2021, IPTL kupitia mwanasheria wake, Joseph Makandege, ilipinga sakata hilo kujadiliwa bungeni jijini Dodoma, kwa madai kuwa wanaolijadili vibaya wana mgongano wa kimaslahi.

IPTL inayomilikiwa na Harbinder Singh Sethi, inadaiwa kufungua kesi mwaka huu, ikiitaka TANESCO iilipe mabilioni ya fedha, ikidai ilikiuka makubaliano waliyoingia ya uzalishaji na ununuzi wa umeme.

Hata hivyo, kesi hiyo inadaiwa kuendeshwa katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, kimya kimya baada ya IPTL kuomba iendeshwe kwa siri ikidai taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: