Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rubani mdogo Mtanzania anayerusha ndege afunguka - Video

Video Archive
Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi karibuni tulikuletea simulizi ya Ndege ya kivita ya Ukraine, MiG-29 Fulcrum inayoongozwa na rubani aliyebatizwa jina la The Ghost of Kyiv (Mzimu wa Kyiv) ambayo ilikuwa gumzo. Ndege hiyi ilipata umaarufu mkubwa kutokana na oparesheni za kijeshi inazozifanya katika Jiji la Kyiv ambapo ilisemekana kuziangusha ndege sita za kivita za Urusi.

Inaelezwa kwamba ndege sita za Urusi zilitunguliwa Februari 24, 2022 muda mfupi baada ya Urusi kuanza mashambulizi ya anga dhidi ya serikali ya Ukraine na kuanzia hapo, The Ghost of Kyiv amepata umaarufu mkubwa na kuungwa mkono na wananchi wengi wa Ukraine.

Tukiachana na stori hiyo, turudi hapa Bongo na tukutane na simulizi nyingine ya binti Mtanzania mwenye umri mdogo ambaye anaweza kuendesha helkopa. Huyu si mwingine bali ni luteni Usu Hasnat Akbar.

Ni binti ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya kuhitimu masomo yake ya urubani Afrika Kusini. Amesimulia changamoto alizokutana nazo pamoja na mambo mengine mengi. Karibu umsikilize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live