Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kumalizia kujenga msikiti mkubwa wa Wilaya ya Chato uliowekwa jiwe la msingi na hayati Dk John Pombe Magufuli ambao umeshindwa kukamilika kwa wakati.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda ameeleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini wa Mkoa wa Geita, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya Kanda ya ziwa.
"Moja ya kipaumbele changu ni kuona Mungu anaabudiwa nimeongea na Mwenyekiti wa chama, Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataumalizia msikiti uliowekwa jiwe la msingi na hayati John Magufuli, hivyo amenitaka niondoke na ramani ya ya msikiti huu, gharama ya kumalizia kujenga, na nikutane na wakandarasi walioanza kujenga msikiti huu, ili waendelee kujenga msikiti," amesema Makonda.
Viongozi hao wa dini walimuomba kiongozi huyo kuwawezesha, ili kumaliza ujenzi wa msikiti huo kw asababu umeanza kuharibika na kwa sasa umegeuka kutumika kama sehemu ya wahalifu kujificha.