Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kugharamia matibabu ya mtoto aliyekatwa koromeo

Dada Wa Kazi Aliyedaiwa Kumchinja Mtoto Wa Bosi Wake Akamatwa.png Rais Samia kugharamia matibabu ya mtoto aliyekatwa koromeo

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema atalipia gharama zote za matibabu kwa mtoto aliyekatwa na kitu chenye ncha kali shingoni

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu  amesema mtoto huyo Maliki Hashimu (5) mkazi wa Goba mkoani Dar es Salaam anatibiwa katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili kutokana na majeraha yalitenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti hivyo kusababisha ashindwe kupumua vizuri.

Aliongezea kuwa wataalamu bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili -MNH wamemfanyia upasuaji mkubwa mtoto huyo uliochukua saa nne ili kurekebisha njia ya hewa, sanduku la sauti, matezi aliyopata changamoto kwenye shingo na kutibu jereha la nyuma ya shingo.

“Jeraha la mbele ya shingo liliharibu tezi la mbele kwa kulikata katikati na kusababisha mtoto huyo kuvuja damu kwa wingi” alisema  Waziti Ummy.

SOMA: UTPC waanzisha kampeni dhidi ya ukatili wanawake, watoto Pia mtoto huyo anapata maumivu kutokana na jeraha alilokatwa mbele ya shingo ambako hewa inayotoka kwenye mapafu hupita ili iweze kwenda kwenye sanduku la sauti kumuwezesha kuhema na kuzungumza.

Hospitali ya Taifa Muhimbili ilimpokea mtoto huyo usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii na kwa sasa yupo chini ya uangalizi maalumu akiendelea kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo Ummy amewapongeza watoa huduma kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia wananchi kwa weledi.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilisema linamtafuta msichana wa kazi, Clemensia Cosmas kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto huyo.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ilisema mtoto huyo alijeruhiwa Julai 15 mwaka huu saa 12 jioni katika eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni. Kamanda Muliro alisema mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda kosa hilo hivyo anatafutwa.

Baba wa Malick, Hashim Mohammed alisema Malick ndiye aliyemtaja binti huyo wakati mama yake alipomuuliza ni nani alimjeruhi. Inadaiwa kuwa Clemensia ni mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma na amefanya kazi kwenye familia ya Mohammed kwa miezi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live