Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia azuru kaburi la Hayati Magufuli

Samia Kaburi Jpm Rais Samia azuru kaburi la Hayati Magufuli

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezuru na kuomba dua kwenye Kaburi la Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Samia amezuru kaburi hilo leo, Jumamosi tarehe 15 Oktoba, 2022 wakati akiwa ziarani mkoani humo baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera.

Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2022 wakati akipatiwa matibabu jijini Dar es Salaam na Machi 19, mwaka huo huo, Samia aliapishwa kushika wadhifa huo kutokana na katiba ya Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live