Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia azindua barabara ya Km 32.2 KLM

Video Archive
Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia, Mapema Oktoba 15, 2021 amezindua miradi ya maendeleo mkoani Kilimanjaro, akianza na ufunguzi wa barabara ya Sanyajuu hadi Elerai yenye umbali wa kilomita 32.2.

Ujenzi wa barabara hiyo ulianza tangu mwaka 2016 na umegharimu jumla ya bilioni 62.7 hadi kukamilika kwake.

Rais Samia amesema kuwa ujenzi huo unafanyika kwa awamu, na kuwa tayari zimeshafinyika awamu mbili iliyobaki ni awamu ya tatu itakayokamlisha barabara hiyo.

"Niwapongeze kwa barabara hii, barabara hii ilikuwa ni kero ya siku nyingi, tumefanya kwa awamu na hii ni ya pili na iliyobaki ni awamu ya tatu na usanifu umeshafanyika kilichobaki ni kutoa fedha" Rais Samia

Viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki zoezi hilo akiwemo Waziri wa Ujenzi, Prof Makame Mbarawa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Barabara hiyo itasaidia kukuza uchumi kwa kuimarisha shughuli za utalii katika Mlima Kilimanjaro, pia inaunganisha kwa ukaribu mkoa huo na Arusha pamoja na nchi jirani ya Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live