Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aweka jiwe la msingi hospitali ya Mawenzi Kilimanjaro

Video Archive
Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia, Mapema Oktoba 15, 2021 ameweka jiwe la msingi katika Hopsitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro wakati akizindua jengo la Mama na Mtoto ambalo limefikia asilimia 70 kukamilika.

Ujenzi wa jengo hilo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 6 ambazo zimetolewa kwa awamu mbili na tayari fedha za awamu ya kwanza zimeshatolewa.

"Najua kulikuwa na mkwamo kidogo, ila tayari tumeshaweka bilioni 3, na zilizobaki tutazimalizia, jengo hili halikuwa na hadhi inayofaa kwa maana ya hospitali" Rais Samia

Mbali na hayo, Rais Samia amewataka watumishi hao wa umma kufanya kazi kwa bidii kwani Serikali imeshaanza kushughulikia maslahi yao pamoja na kuwapandisha vyeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live