Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia atumbua 'wote' Mambo ya Nje

Rais Samia Atumbua 'wote' Mambo Ya Nje.png Rais Samia atumbua 'wote' Mambo ya Nje

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan unaweza sema ametembeza fagio la chuma katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kutengua uteuzi wa Waziri na manaibu wake wawili.

Taarifa za utenguzi huo imetolewa jana Julai 21, 2024 kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, January Makamba uteuzi wake umetenguliwa huku nafasi yake ikichukuliwa na Balozi Kombo aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia ameteuliwa kuwa Mbunge.

Katika wizara hiyohiyo, Rais Samia ametengua uteuzi wa Stephen Byabato aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pia, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk naye katika taarifa ya Ikulu inasema nafasi yake inachukuliwa na Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cossato Chumi.

Hata hivyo, saa chache kabla ya uteuzi huo, Balozi Mbarouk aliandika barua ya kujiuzulu ubunge kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live