Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia ataka mwongozo wa utambuzi wa machifu ukamilike

Samia Hangaya Rais Samia ataka mwongozo wa utambuzi wa machifu ukamilike

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameilekeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kukamilisha Mwongozo wa Utambuzi wa Machifu na Viongozi wa Kimila katika Wilaya na Mikoa utakaoainisha majukumu yao wa kimila na kijadi.

Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo Julai 20, 2024 wakati akizungumza na Viongozi wa Kimila na Machifu kutoka Tanzania nzima kwenye hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

Amesema Viongozi wa Kimila na Machifu wana mchango mkubwa katika kulinda maadili na kutatua changamoto za kimaadili katika jamii licha ya kuwa yanashughulikiwa katika ngazi ya Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live