Wakazi wa kitongoji cha kukiyugu, waliopo katika kijiji cha Kiabakari Kata ya Kukirango Wilaya ya Butiama wamemshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea huduma ya maji kupitia mradi mkubwa wa maji wa Mugango - Kiabakari kwani kabla ya mradi huo, wakazi walikuwa wanapata changamoto ya maji.
Mradi huo ambao umeshaanza kutoa huduma ya maji kwa hadi sasa upo asilimia 98.7 na unatekelezwa kwa gharama ya zaidi Bilioni 70, fedha kutoka Serikali ya Tanzania, BADEA na Saudi Fund (SFD) na utakwenda kuwanufaisha wakazi zaidi ya 233,033 katika Halmashauri za Wilaya tatu ambazo ni Musoma, Butiama na Bunda.
Kazi ambazo zinatekelezwa katika mradi huu ni pamoja na
1.Ujenzi wa choteo la Maji ( Water intake ) lenye uwezo wa kuzalisha maji mita za ujazo 35,000 kwa siku.
2.Ujenzi wa Mtambo wa kutibu maji ( Water Treatment Plant ) wenye uwezo wa kutibu maji mita za ujazo 17,500 kwa siku.
3.Ujenzi wa tenki la majisafi ( Clear Water Tank ) lenye ukubwa wa mita za ujazo 2400.
4.Ujenzi wa vituo vya kusukuma maji ( Pumping Station ) tatu
5.Ujenzi wa jengo la ofisi katika eneo la Mugango.
6.Ujenzi wa jengo la ofisi Mamlaka ya maji katika eneo la Kiabakari.
7.Ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji ambayo ni Kong Hill 500m^3, Bumangi 1000m^3, Butiama 2500m^3 na Kiabakari 3000m^3.
8.Ulazaji wa bomba kuu lenye
urefu wa km 47
9.Ulazaji wa mabomba ya usambazaji urefu wa km 140
10.Ujenzi wa vituo 40 vya kuchotea maji na maghati 8 ya kunyweshea mifugo.
11. Ununuzi wa dira za maji 2000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Mugango - Kiabakari Eng. Cosmas F. Sanda, amewaasa wakazi wa Mugango, Kiabakari na Butiama kufika Ofisini kwa ajili ya huduma ya maunganisho mapya kwani Vifaa vya maunganisho mapya vipo ofisini na kisha kuwataka kuulinda mradi huo kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.