Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Tanzania amemshukuru Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutosimamisha shughuli za kiuchumi wakati wa janga la Covid 19 na kusema hatua hizo zimesaidia uchumi wa Tanzania kutoshuka kwa sana ukilinganisha na Mataifa mengine.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akizungumza na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (TAHLIFE) leo February 11,2023 Ikulu Chamwino Dodoma “Dunia imekumbukwa na mambo matatu makubwa, Uviko- 19, miaka miwili Dunia kama ilisimama hakukuwa na uzalishaji viwandani wala shughuli za maendeleo, baada ya maradhi kuondoka Dunia kama imeanza upya, viwanda vimeanza upya, chumi zimeanza kujengwa upya”
“Nataka hapa kwa pamoja tumshukuru Marehemu John Pombe Magufuli yeye alisema sisi hatusimamishi kitu kwasababu hatuna uwezo wa kulisha Watu wote hawa kila Mtu atoke akajitafutie riziki lakini tuchukue tahadhari, kwa maana hiyo uchumi wetu haukushuka sana kama ulivyoshuka kwa wenzetu Nchi za jirani ndio maana hatukutetereka sana”
“Uchumi wetu ulikuwa unakua kwa 7% lakini yalipoingia maradhi tumeshuka mpaka 4% lakini kuna Nchi za jirani walishuka hadi 2% hadi 3% kwahiyo sisi tulikwenda vizuri, kwahiyo Dunia imekumbwa na maradhi, mabadiliko ya Tabia Nchi na sasa sio mabadiliko ya Tabia Nchi ni mabadiliko ya Tabia Dunia.”