Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi kilele cha UWT Taifa

SAMIA 6 Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe ya maadhimisho ya Jumuia ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT ) Taifa Oktoba 23,2021 Rufiji mkoani Pwani.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhuduriwa na zaidi ya wanawake 700 kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Pwani ambao watasindikizwa pia watu wengine wakiwemo wanaume, viongozi mbalimbali wa chama hicho na Serikali ikiwa ni sehemu pia ya kumuenzi muasisi wa umoja huo hayati Bibi Titi Mohamed ambaye wazazi wake ni wazawa wa Rufiji mkoani Pwani.

Menyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka amesema hayo leo Alhamis Oktoba 21, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha juu ya maadhimisho hayo.

Kabaka amesema Rais Samia ataungana na wanawake hao zaidi ya 700 ambao kati yake 500 tayari wamethibitisha kushiriki katika kilele hicho.

Alisema lengo la kupeleka Rufiji sherehe hizo za maadhimisho ya wiki ya UWT ni katika kumuenzi aliyekuwa muasisi wa UWT Taifa Hayati Bibi Titi Mohamed ambaye pia alikua mwanachama mwenye kadi namba 16 ya chama.

"Kuanzia kesho Oktoba 22 UWT Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Taifa Mama Kabaka watakwenda kutoa misaada mbalimbali ikiwemo taulo za kike katika Shule za Sekondari za wasichana ikiwemo Ikwiriri, watafanya usafi wa mazingira na watatembelea katika vituo vya afya na kutoka mashuka na sabuni,"amesena na kuongeza

"Misaada hii itakuwa ni kumbukumbu yetu kwao kwa kumkumbuka muasisi wa UWT Hayati bibi Titi Mohammed ambaye ni mazaliwa wa Rufiji."

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakari Kunenge amewashukuru UWT Taifa kwa kufanya maamuzi ya kupeleka sherehe hizo wilayani Rufiji kwani itachangia kutangaza Mkoa wa Pwani na kutangaza katika fursa za kitalii kwa ujumla na pia amewahakikishia wananchi kuwa usalama upo wa kutosha.

Chanzo: mwananchidigital