Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Nani anatumia Ubungo Plaza?

Samia Uwanjani Rais Samia: Nani anatumia Ubungo Plaza?

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Mashirika kutimiza wajibu wao ili kuongeza wawekezaji wengi Nchini, amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kwenye Ukumbi wa AICC, leo Agosti 28, 2024.

Rais Samia amesema hayo wakati akishiriki Ufunguzi wa kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), leo tarehe 28 Agosti, 2024.

Amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikifanya kazi vizuri itasaidia kuvuta wawekezaji wengi kuja Nchini kwa kuwa uratibu wa kodi utakuwa vizuri

Aidha, amesema “Mfano TBS (Shirika la Viwango Tanzania) wakiwa makini sana kusimamia viwango vya uzalishaji wa ndani watasaidia wazalishaji kufikia viwango vya kimataifa, huo utakuwa mchango wa kuzuia wale wanaoleta bidhaa kwa viwango vya chini wasilete kwa kuwa wa kwetu wamefikia viwango vya kimataifa.”

"Kauli mbiu hii nadhani ni kauli mbiu ni sahihi kujadiliwa katika kikao hiki, nami niwatie moyo mjadili kwa mapama, msikilize uzoefu, mtoe maoni yenu. Baadae huko tuje na mpango tunakwenda vipi tunapoa amua kuvuka lakini lazima tuwe na mkakati tunakwenda vipi.

"Lakini pamoja na hayo ni vizuri kukumbuka kuwa uwekezaji nje ya Nchi utakuwa na maana zaidi iwapo wananchi wetu watakuwa na uhusiano na ufanisi wa mashirika haya ndani ya nchi. Yaani tuonyeshe tija ndani.

"Niseme pia kwamba kujadilia kuhusu kutafuta fursa, naomba pia mjadiliane namna mashirika yetu yakavyoweza kuchangia sekta binafsi kuyafikia masoko binafsi.

"Sasa kuna mashirika ambao yanaweza kufanya kazi hapahapa ndani kuboresha mashirika mengine yaweze kufanya uzalishaji vizuri zaidi. tuchukulie shirika kama TBS, TBS wakiwa makini sana kusimamia viwango vya uzalishaji wa ndani na kuwafanya wazalishaji wandani waweze kuwasaidia kufikia viwango vya kimataifa watakuwa wametoa mchango mkubwa sana.

"Mchango wa kwanza ni kuzuia wale wa nje wanaotuletea bidhaa za viwango vya chini visiingie huku ndani TBS wawe makini na wazuie. wawazuie wasilete bidhaa za viwango vya chini kwa sababu wakwetu wamefikia viwango vya kimataifa.

"Lakini pia TRA kwa mfano wakifanya kazi yao vizuri sana kuwafanya wawekezaji wanatoka nje kuja ndani walipe viwango ambavyo havileti malalamiko na hakuna kuchukua mashine za watu hii tutavuta wawekezaji wengi sana waje ndani kwa sababu uongozi wa kodi utakuwa umekaa vizuri sana.

"Lakini vilevile TRA wakiwasidia wa ndani wakuwe vizuri na waweze kufanya biashara na kuliplace wanje wanaokuja kufanya biashara ndogo ndani ambayo mtanzania anafanya watakuwa wametusaidia wenyewe sana kukuza biashara ndani yetu na kukuza mapato yetu.

"Wasio wangu kwenu pamoja na kwamba nimesema mshirikiane, muwekeze mfanye mabadiliko muende vizuri lakini tufanye baada ya kufanya utafiti wa kutosha halafu tuamue kuwekeza.

"Kwa nini nasema hivi kwa sababu kuna mashirika kwa utashi tu wa kisiasa pengine wameingiza pesa pahali ambazo hizo pesa hazirudi na sina kigugumizi nimesema si kama mara 2 au mara 3. Mfano wangu mkubwa ni kama Ubungo. Ubungo Plaza ilivyofunguliwa ilikuwa kila mtu hee Ubungo Plaza mikutano yote tunaswaga wote tunawekwa huko lakini sasa hivi nani anatumia Ubungo Plaza."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live