Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Magufuli alinifundisha mengi, halitaharibika jambo

Magufuli Na Samia Rais Samia na Magufuli

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani kuelekea mkoni Kagera amesimama katika kijiji cha Bwanga mkoani Geita na kuongea na wananchi wa kijiji hicho.

Akiongea na wananchi hao Rais Samia amesema katika awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli alipata fursa ya kujifunza mambo mengi sana chini ya kaka yake Hayati Magufuli ambayo yote amebainisha kuwa yatatekelezwa katika awamu yake.

“Awamu iliyopita nilikuwa Makamu wa Rais chini ya Kaka yangu Marehemu John Pombe Magufuli alinifundisha mambo mengi sana, niliisoma dhamira yake vizuri sana, jinsi ya kuipeleka nchi hii.

"Nataka niwahakikishie dhamira ileile tunakwenda nayo maendeleo kwa wananchi hakuna hata mradi mmoja tuliouanza nyuma ambao utakufa na hatutauendeleza lakini na ile mipya inayokuja ni kwa dhamira ileile, kwahiyo niwahakikishie halitaharibika jambo,” alisema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live