Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Kumwaga Barabara, Kivuko Kikubwa Kigamboni - Video

Video Archive
Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea kilio cha wananchi wa Kigamboni kuhusu changamoto ya barabara na kumtaka Mbunge wa Jimbo la Kigamboni kusaidia kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23.

Rais Samia amesema hayo leo Desemba 06, 2021 awakati aliposimama kuzungumza na wananchi wa Kibada Kigamboni akielekea kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Elsewedy Electric Africa Limited kilichopo Kisarawe 11, Kigamboni.

Kauli ya Rais imekuja baada ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile kumweleza shida za wananchi wa Kigamboni.

“Kigamboni tuko nyuma sana katika miundombinu ya barabara. Katika barabara za Tarura, asilimia 37 tu ya barabara zimepigwa lami. Na katika asilimia 100 ya barabara za vumbi mkoa wa Dar es Salaam, asilimia 50 zipo wilaya ya Kigamboni.

"Wananchi wa Kigamboni wanashukuru sana kwa ujenzi wa Daraja la Nyerere. Ni mkombozi mkubwa. Changamoto ni tozo. Daladala moja inatozwa Sh5,000 ikienda mara kumi kwenda na kurudi ni Sh100,000 kwa siku. Hapo hajaweka mafuta, hajaweka hela ya tajiri.

“Nakuomba sana Rais twende tukaliangalie jambo hili. tuangalie jinsi gani tunaweza kuleta nafuu kwa wananchi wa Kigamboni na kufanya maisha yawe mepesi. Wananchi wamenituma hilo niweze kulifikisha kwako,” amesema Ndugulile.

Aidha, Mhe. Rais ameahidi kuleta Kivuko kingine kipya Kigamboni.“Suala la uchakavu wa vivuko, vinavyovusha watu Kigamboni, niwaambie kuwa hili lipo ndani ya mipango yetu tunalifanyia kazi tuone uwezekano wa kupata kivuko kikubwa chenye kuchukua watu wengi na mizigo mingi ili kupunguza safari za vivuko vidogo kwenda na kurudi,” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live