Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu TPA - Video

Video Archive
Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rais Samia Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu TPA – Video March 28, 2021 by Global Publishers



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumapili, Machi 28, 2021 amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.

Rais Samia amefikia uamuzi huo baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko.

“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” amesema Rais Samia.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8​ ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Chanzo: globalpublishers.co.tz