Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli umeisafisha CCM na kuivua gamba – Afande Sele

4832 Afande Sele TZW

Sat, 17 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele kabla ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi(CCM) Mapema leo amemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa amekisafisha chama hicho na kukivua gamba.



Afande Sele ameyasema hayo leo Machi 15, 2018 wakati Rais Magufuli akizindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro.

“Rais chama chako cha mapinduzi umekisafisha umekivua gamba na ni chama ambacho kimerudi katika uimara wake kama chama cha wanyonge kwa jinsi ambavyo Mhasisi wetu baba wa Taifa alitaka kiwe ndivyo ambavyo umekifanya chamacha mapinduzi leo kimekuwa hivyo Mh. Rais naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi nikuhakikishie kwamba nimeamua kujiunga upande mmoja na wewe ili nisiache na jahazi hili,” amesema Afande Sele.

“Kwasasa hivi Tanzania kama dereva gari limetulia na linakwenda na mimi kama abiria niache ninywe soda yangu kwa furaha kwa furaha na amani kwasababu naamini chombo chetu kinakwenda salama na sipendi kesho historia ini hukumu niwe miongoni mwa wale ambao hawakuchangia chochote.”

Chanzo: bongo5.com