Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli amtolea nje Mbunge TMK "hizo hela mtalipa wenyewe" (+video)

Video Archive
Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mkopo wa Sh19 bilioni uliotolewa na benki ya CRDB kwa halmashauri ya Temeke.

JPM ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 26, 2021 katika ziara yake jijini Dar es Salaam baada ya mbunge wa Temeke (CCM), Dorothy Kilave kuomba Serikali iwasaidie kulipa mkopo huo unaowagharimu Sh4.8 bilioni kila mwaka.

“Yaani Serikali ikalipe mkopo ambao haikuhusika, haya ni mambo ya ajabu. Mlienda kuzungumza wenyewe na benki mmeshindwa kulipa mnataka Serikali ilipe. Kuna Manispaa ngapi kwa hiyo ziwe zinafanya mikopo ya wizi halafu serikali ilipe. Hilo mtalibeba wenyewe, kwanza ni kukosa nidhamu.” Magufuli

“Hakuna hela itakayotolewa na serikali labda kutuma wachunguzi kuchunguza kujua hizo fedha zinarushwa kiasi gani, namuelekeza kamanda wa TAKUKURU kuchunguza hawa naona kuna ufisadi mkubwa unaelea,” Magufuli.

Chanzo: millardayo.com