Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewakumbusha wakazi wa Iringa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za Urais ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda.
Rais Magufuli ameyasema hayo mkoani Iringa wakati anafanya uzinduzi wa barabara ya Iyovi ambapo ameeleza kuwa yote aliyoyaahidi katika ilani ya uchaguzi watayatekeleza.
“Nataka niwaahidi kwenu yale yote niliyowaahidi katika ilani ya uchaguzi yale yalioahidiwa na waheshimiwa Wabunge na Madiwani wakati tukijinadi katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi tutayatekeleza kwa kushirikiana na nyinyi katika kuhakikisha kwamba tunawaondolea wananchi kero na kujenga Tanzanoia mpya kwaajili ya maendeleo ya Watanzania wote ,” amesema Rais Magufuli.
Ameongeza “Kama mnakumbuka moja ya ahadi kubwa tulizozitoa wakati wa kampeni ilikuwa ni kujenga uchumi ya viwanda nakumbuka pia tulitaja na kuelezea sifa za viwanda tulivyolenga kuvijenga kwanza vyenye kuajili watu wengi pili vyenye kutumia malighafi zenye kupatikana hapa nchini ili mazao yetu na Rasilimali zingine tulizonazo zipate masoko tatu ambazo bidhaa zake zinatumika hapa nchini na pia kuweza kuuzwa nje ya Nchi, lengo hapa nikupunguza kuwa tegemezi na kuuza bidhaa nje ya nchi lakini pia kuipa nchi yetu fedha za kigeni.”