Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli "Uchaguzi sasa umekwisha" (+video)

Video Archive
Thu, 5 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amesema kuwa sasa hivi suala la uchaguzi limekwisha na kilichopo kwa sasa ni kujenga na kutengeneza maendeleo ya Taifa hilo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati akihutubia Watanzania mara baada ya kula kiapo cha kuliongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

“Uchaguzi sasa umekwisha, jukumu kubwa lililopo mbele yetu ni kuendeleza jitihada za kujenga na kuleta maendeleo kwa Taifa letu na niwahakikishie kuwa kiapo nilichoapa na alichoapa makamu wangu tutahakikisha na kukienzi kwa nguvu zote” Rais Magufuli,

Niwashukuru na kuwapongeza Watanzania kwa kuonesha utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi, kama mjuavyo kwenye baadhi ya nchi uchaguzi umekuwa chanzo cha uhasama, sisi Watanzania tumevuka mtihani huo salama na kuthibistha ulimwengu sisi ni wapenda amani” Rais Magufuli 

Chanzo: millardayo.com