Murugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ameeleza katika Uzinduzi wa Azimio la Kagera jana December 16, 2017 kuwa kuna haja wa wadau wote wa fursa za maendeleo kukaa kwa pamoja kuangalia changamoto zinazowakabili na kutafuta ufumbuzi kisha kupanga maazimio ya pamoja ya utekelezaji.
Aliongeza kuwa katika kuzungumzia kukua kwa uchumi ni lazima watu binafsi waone uchumi wao ukikua, kwani kukua kwa uchumi wa mtu binafsi hupekekea uchumi wa nchi pia kukua kwa urahisi na uharaka.
“Lazima tutengeneze mazungumzo ya pamoja ya watu ambao ni Maprofesa wa chuo kikuu lakini pamoja na wahitimu wa darasa la saba ambao wana uzoefu unaofanana na Maprofesa wa chuo kikuu.” – Ruge Mutahaba
FURSA 2017: “HAKUNA WA KUKULETEA CHAKULA, LAZIMA UKITAFUTE ” RUGE MUTAHABA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA