Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtwara: Kopeni kwenye taasisi rasmi kuepusha matatizo

FEDHA RC Mtwara: Kopeni kwenye taasisi rasmi kuepusha matatizo

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amewahimiza wananchi mkoani humo pale wanapotaka kukopa mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi waende kwenye taasisi rasmi zilizosajiliwa kisheria kujiepusha na matatizo mbalimbali.

"Nitumie nafasi hii kuendelea kuwashauri wananchi wanaohitaji mikopo kwenda kukopa kwenye taasisi rasmi zilizosajiliwa kisheria kwa ajili ya usalama wa fedha zao,” amesema Kanali Sawala

Aidha Kanali Sawala amewaasa watoa huduma ndogo za fedha mkoani humo na kwingineko kuhakikisha kuwa wamesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 pamoja na kanuni zake za mwaka 2019, na kuonya kuwa watakaotoa huduma hizo bila kufuata sheria watawajibishwa kwa mujibu wa sheria tajwa.

Kanali Sawala amesema hayo alipokuwa akizungumza na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na taasisi shiriki, waliomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha mafunzo kuhusu fedha yatakayoendeshwa katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara. 13h

mkundabaraka79's profile picture Tatizo rasimi na mikopo haviendani, short and clear, mkifatilia undani wake mtakuja kivingine na elimu itakayowafaa wakopaji kufikia malengo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live