Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mghwira afiwa na baba yake

21194 Rc+pic TanzaniaWeb

Mon, 8 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amefiwa na baba yake mzazi, Elisha Mghwira leo Jumamosi Oktoba 6, 2018.

Akizungumza na MCL Digital leo jioni mkuu huyo wa mkoa amesema baba yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mfumo wa chakula.

"Baba amefariki kwa tatizo la mfumo wa chakula," amesema Anna na kubainisha kuwa msiba upo Kiluvya jijini Dar es Salaam nyumbani kwa kaka yake.

Amesema Jumatatu Oktoba 8, 2018 watasafirisha mwili kwenda nyumbani kwao mkoani Singida, kwamba mwili wa baba yake umehifadhiwa hospitali ya Mloganzila jijini Dra es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz