Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira amemuagiza Mkuu Wilaya ya Taita Taveta nchini Kenya kuwaachia huru Watanzania saba wanaoshikiliwa nchini humo kwa zaidi siku 14 kwa makosa mawili ya kutovaa barakoa na kuingia bila kibali.
Akuzungumza mara baada kikao cha kutafuta suluhu iliyoshirikisha pande zote mbili ya Tanzania na Kenya iliyofanyika katika mpaka Holili Wilayani Rombo na kuhudhuriwa na Wakuu wa Wilaya Taita Taveta, Mkuu Wilaya Rombo, Mwanga na Moshi.
Dkt. Mghwira amesema kuwa kikao hicho ni kuhusiana na kushikiliwa waendesha boda boda raia wa Tanzania 15 walioshikiliwa Taveta makosa mawili ambapo nane walifanikiwa kutoka baada kutimiza masharti huko wengine saba walishindwa kutimiza masharti hayo.
Amesema kuwa baada kukamatwa walipigwa faini kwa kila kosa ambapo kosa la kwanza ni yakuingia bila kibali ambayo faini yake ni Sh za Kenya 20,000 kosa la pili Kutovaa barakoa Shilingi za Kenya 30,000 sawa 1,000,000 za Tanzania.
“Tumekaa tukajadili lakini tumeona ni makosa tu yakawaida ya kimazoea ya kibiashara kwa sababu Wakenya wanaingia bila kufuata taratibu tena bila masharti wanachukua bidhaa lakini Watanzania wakiingia tu upande wa kenya ni kosa, “ Dk. Mghwira
ASKARI POLISI AJINYONGA KWENYE NYUMBA INAYOJENGWA “ALIKUWA MTU WA WATU”