Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RAS Kilimanjaro na dereva wake wafariki kwa ajali + VIDEO

Video Archive
Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda na dereva wake, wamefariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la KIA wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba imetokea leo Juni 18, 2024 majira ya saa nane mchana.

Inaelezwa kuwa, muda mfupi kabla ya ajali hiyo, katibu tawala huyo alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Tanzania Web inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu. Mungu azilaze roho za marehemu hawa mahali pema peponi, amina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live