Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Popo wazua mjadala Bungeni

Popo Pic Bnbnnnn Popo wazua mjadala Bungeni

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum,William Mgaya amehoji bungeni ni lini serikali itaondoa popo waliopo maeneo ya Upanga, Dar es Salaam ili kulinda afya za wakazi wa eneo hilo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Danstan Kitandula, amesma wizara imeendelea kudhibiti popo katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya soroveya ya kuangalia ukubwa wa tatizo, maeneo yaliyoathirika, mbinu gani ambazo ni rafiki kwa mazingira zitumike kudhibiti na pia kubaini aina ya popo wanaosumbua.

‘’Imebainika kuwa kuna aina mbili (2) ya popo wanaosumbua, ambao ni popo wanaokula matunda (hawa wanaotumia miti kama maeneo yao ya makazi) na popo wanaotumia mapango au magofu ya nyumba kama makazi yao.

‘’Katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, majaribio ya dawa tano (repellents) za kunyunyizia ili kufukuza popo katika makazi yao (roosting sites) zilitumika. ‘’Kati ya dawa hizo; dawa mbili (Napthalene na Bat CRP) zimeonekana kuwa na uwezo wa kuwafukuza popo hao na juhudi zaidi zinaendelea kwa kushirikiana na wadau kwenye maeneo husika,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: