Jeshi la Polisi limefanya upekuzi nyumbani kwa aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob maarufu kama Boni Yai.
Polisi walifanya upekuzi huo jana Septembe 18, 2024 mara baada ya kumkamata Boni na kumpeleka katika kituo cha Polisi Oystebay kisha baadaye kwenda maeneo ya Mbezi, Msakuzi usiku ambapo walimaliza upekuzi huo majira ya saa 5:45.
Upekuzi huo ulianza saa 2 usiku, na kwa zaidi ya saa tatu, Makachero wa Polisi wamepekua maeneo mbalimbali ya nyumba hiyo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa, hawachukua kitu chochote katika upekuzi huo na walipomaliza, walimchukua Boni na kumrudisha kituo cha Polisi Oysterbay.
Awali zilisambaa taarifa mitandaoni kuwa Boni alitekwa lakini hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake David Misime, lilikanusha taarifa hizo na kueleza kwamba anashikiliwa na polisi kwa makosa ya kijinai.
Taarifa hiyo ilieza kawa, taarifa za kwamba Boni ametekwa zipuuzwe.