Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Afrika

Nchi

Kijamii

Polisi kununua magari 265

Magari Serikaliiii Polisi kununua magari 265

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema inakusudia kununua magari 265 ikihusisha magari 147 ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya zote kote nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 72 kwa ajili ya mpango huo ikiwa ni mkakati wa kuboresha vitindea kazi kwa Jeshi la Polisi.

Tayari Jeshi hilo limepokea magari 44 kati ya 200 ambayo yamepangwa kuwasili muda wowote. Kiasi hichho pia kitahusika katika ununuzi wa magari ya polisi kuanzia ngazi ya Taifa hadi Vituo vya Polisi.

“Kiasi cha Sh bilioni 15 zimeshapokelewa na taratibu za ununuzi unaendelea,” Masauni amewaambia wabunge mjini Dodoma.

Vilevile, Masauni amesema Sh bilioni 11.6 zimepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa boti 10 za kufanya doria maeneo ya bahari na maziwa kote nchini, pikipiki 19 za kuongoza misafara ya viongozi na magari 24, ambapo mzabuni ameshapatikana.

Katika mwaka 2024/25 jumla ya Sh bilioni 36 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa magari 181. Aidha, Sh bilioni 118.1 zimetengwa ili kununua vifaa vya kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live