Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Padri Katoliki na wenzake nane wafikishwa mahakamani mauaji ya Asimwe - VIDEO

Video Archive
Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ATU Tisa wamefikishwa mahakamani ya hakimu mkazi mfawidhi Mkoa wa Kagera kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mwenye ualibino Asimwe Novart aliyeuliwa na kukatwa viungo vyake vya mwili na kisha mwili wake kutekeleza kwenye kalavati.

Watuhumiwa waliofikishwa katika mahakama hiyo ni pamoja na Padre Elipidius Rwegoshora wa kanisa katoliki Jimbo la Bukoba na baba wa mtoto Asimwe Novart Venant.

Watu wengine ni Ramadhani Selestine, Nurdin Masoud, Rwenyagira Burukadi, Dunstan Burchard, Faswiu Athman, Gozbert Alchard na Dezdery Evergist ambao wote kwa pamoja wamesomewa shitaka Moja la mauaji ya kukusudia.

Washitakiwa hao Tisa wamesomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Mkoa wa Kagera Waziri Magumbo akisaidiana na wakili mkuu wa serikali Erick Mabagala mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson.

Asimwe Novath alipotea katika mazingira ya nyumbani Mei 30, 2024 na mwili wake kupatikana ukiwa umenyofolewa viungo Juni 17,2024 na kusababisha kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live