Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha walioungana Maria na Consolata wafariki Dunia, Rais Magufuli alizwa na kifo chao

Video Archive
Mon, 4 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

/>

Maria na Consolata Mwakikuti enzi za uhai wao

 

Mapacha hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya moyo walilazwa tangu mwezi Disemba mwaka jana katika hospitali ya mkoa ya Iringa.

Hata hivyo, baadae walihamishiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo walikaa kwa miezi miwili kwa ajili ya matibabu mpaka waliporuhusiwa kurejea tena Iringa mnamo Mei 17, 2018 .

Mapacha hao walizaliwa wilayani Makete mkoani Njombe mwaka 1996 na walihitimu darasa la saba katika shule ya msingi Ikonda, kisha wakajiunga na shule ya Maria Consolata iliyopo Kilolo mkoani Iringa ambapo walihitimu kidato cha nne.

Maria na Consolata, walijiunga na shule ya Sekondari ya Udzungwa wilani Kilolo na kuhitimu kidato cha sita, ambapo walifanikiwa kusonga mbele na kujiunga na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu) walipokuwa wakisomea fani ya ualimu.

Kufuatia vifo hivyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa salamu za rambi rambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa mapacha hao.



 

 

Loading...
Chanzo: bongo5.com