Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PICHA: Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani

WhatsApp Image 2021 09 21 At 7.24.20 AM 1 660x400.jpeg Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Septemba 20 ,2021 ameshiriki mkutano wa umoja wa Mataifa uliojadili kuhusu athari za Mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikumba dunia na kusisitiza umuhimu wa kutopuuzia juhudi za kukabiliana na janga hilo.

“Tuko katika kipindi ambacho wakati tunapambana na athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchini bado tunataabika na chanamoto kubwa ya sasa ambayo ni Ugonjwa wa Virusi vya Korona, Uviko-19 ambasyo imeangusha sana hali ya Uchumi na kufuta mafanikio yaliyokwisha katika miongozi kadhaa ya kujenga jamii zetu”- Rais Samia

Mhe Rais Samia amesisitiza pia kuwa ingawa watu wengi wanachukulia kirahisi kupanda kwa hali ya joto kama moja ya athari za mabadiliko ya Tabia nchi, bado hali ni kusikitisha kwa nchi kama Tanzania kwani hali hiyo husababisha ukame ambao ni athari mbaya kwa sekta zinazotegemea maliasili kama vile kilimo, uvuvi, na misitu ambazo zinachangia 30% ya pato la Taifa na kuathiri takribani 60% ya Wananchi.

.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grand, walipokutana Jijini New York Nchini Marekani.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa nje ya Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa, Jijini New York Nchini Marekani tarehe 20 Sept, 2021, baada ya kushiriki mkutano uliojadili masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula. Kushoto ni Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York Marekani Balozi Kennedy Gaston.
Chanzo: millardayo.com