Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba ya Tsh. Milioni 200 iliyojengwa kwenye kiwanja cha watu yavunjwa

Video Archive
Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Taharuki ya aina yake imetokea alfajiri ya Oktoba 16, 2021 katika eneo la Mbezi Goigi jijini Dar, baada ya nyumba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 kuanza kuvunjwa kwa kile kilichoelezwa kwamba imejengwa kwenye kiwanja chenye mgogoro.

Mmiliki wa kiwanja hicho, Said Ukwaju anadai kwamba ameshinda katika kesi iliyokuwa mahakamani na kupewa ruhusa na mahakama ya kuvunja nyumba hiyo, ambayo mmiliki wake ni mwanamke anayeitwa Camela Lema.

Global TV imefika eneo la tukio na kuzungumza na mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye ameeleza kwa kirefu kuhusu sakata hilo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz