Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugulile: Watanzania mniombee, hili jukumu la WHO ni zito

Ndugulile 2 1 Ndugulile: Watanzania mniombee, hili jukumu la WHO ni zito

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi mpya wa Kikanda wa Afrika katika Shirika la Afya duniani (WHO) na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile amewaomba wabunge na watanzania kwa ujumla kuendelea kumfanyia sala na dua katika jukumu jipya jipya alilonalo la kuliongoza Bara la Afrika katika shirika hilo.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo wakati akitoa hotuba ya kushukuru baada ya kushinda nafasi hiyo Dkt. Ndugulile amesema jukumu hilo ni kubwa kwake kwa maana limebeba maono ya watanzania na waafrika kwa ujumla.

Aidha amesema kwa kushika nafasi hiyo, anawaongoza waafrika wasiopungua bilioni 1.5 na nchi 45 za Afrika na ataitumikia kwa miaka mitano na kituo cha kazi kitakuwa Brazzaville katika Jamhuri ya Congo.

“Niwaombe tu waheshimiwa wabunge tuendeleze sala na dua kwangu, jukumu hili ni kubwa sana, limebeba maono ya nchi yetu, lakini imebeba maono ya wana Afrika, waafrika wanategemea makubwa sana.” Alisema Dkt. Ndugulile katika hotuba yake.

Dkt. Ndugulile anatarajiwa kuanza kazi rasmi katika nafasi hiyo mwishoni mwa mwezi Februari ama mwanzoni mwa Machi mwaka 2025 ikiwa ni utaratibu wa taasisi za kimataifa kutoa miezi sita ya kujiandaa na hivyo kumpa nafasi ya kuendelea kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kigamboni mpaka kipindi hicho.

“Wengi wamekuwa wanauliza Mheshimiwa Naibu Spika kuwa lini unaanza kazi, utaratibu wa taasisi za kimataifa toka uchaguzi mpaka unaanza kazi unapewa miezi sita. Kwa hiyo natarajia kuanza kazi mwishoni wa Februai au Machi 2025.

“Sasa wale waliokuwa wanahoji Jimbo la Kigamboni lipo wazi, hapana bado lina Mbunge, bado nipo nipo. Na nawashukuru wote wenye nia njema na ambao hawakuwa na nia njema kwa maana wote waliniombea dua na walikuwa wananiunga mkono.” Alisema Dkt. Ndugulile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live