Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wa Magufuli: Mzee hakutaka tujulikane

Magufuli Dominic Ndugu wa Magufuli: Mzee hakutaka tujulikane

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa dada wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aitwaye Furaha Dominic amesema kiongozi huyo aliilea familia yake katika mazingira ambayo hakutaka wajulikane.

Furaha amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online katika kipindi maalum cha Hoja kwa Hoja huku akieleza kuwa jambo hilo limewasaidia kama familia kuishi maisha ya kawaida bila kujali kwamba mzazi wao ni Rais wa nchi.

“Mzee (Magufuli) alituelea katika mazingira ambayo hakutaka tujulikane, na aliaamini kwamba kila mmoja ana bahati na njia zake katika uongozi ama mafanikio, hivyo hakutaka kabisa tujulikane kama ni watoto wake.

“Tumeona watoto wa marais waliopita walikuwa wakijulikana na ni maarufu kuliko hata mawaziri, lakini kwa Magufuli haikuwa hivyo. Tuliishi maisha ya kawaida kabisa, nilikuwa natembea kwa boda boda wala watu hawakujali kwa sababu hawakunijua. Lakini sasa nikipanda bodaboda wananishangaa kwa sababu ninafahamika ni ndugu wa Magufuli.

“Mimi nimefahamika baadha ya kujitokeza kuomba ridhaa ya Ubunge wa Kawe, tena ni baada yay eye mwenyewe kusema. Lakini kabla ya hapo sikuwahi kujulikana kabisa, hata watoto wake wengine wamekuja kufahamika wakati wa msiba wake.

“Kuna siku moja nilipita nikiwa nimebebwa kwenye Bodaboda pale Salender Bridge, maaskari wa Tambaza wakatukamata wakachomoa ufunguo wa pikipiki tukaanguka, pale pale nilimwandikia ujumbe mzee (Magufuli) nikamwabia hawa vijana wa bodaboda wanateseka sana, nikampa ushuhuda.

“Sikusema tu kutokana na tukio lililonikuta bali nililisemea Taifa zima. Mzee aliamuru bodaboda waruhusiwe kuingia mjini mpaka pale ambapo taratibu nzuri zitawekwa. Kwa hiyo alikuwa ni mtu anayesikiliza na kujali shida hasa za wanyinge,” amesema Furaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live