Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndejembi aenda Ardhi, Silaa apewa Habari

Ndejembi Aenda Ardhi, Silaa Apewa Habari.png Ndejembi aenda Ardhi, Silaa apewa Habari

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Awali, alikuwa Waziri Ofisi Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambapo ameteuliwa Ridhiwani Kikwete kuwa waziri.

Ndejembi ambaye ni Mbunge wa Chamwino (CCM), Dodoma amechukua nafasi ya Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Silaa ambaye ni Mbunge wa Ukonga, amechukua nafasi ya Nape Nnauye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Uteuzi huo umefanyika jana Jumapili, Julai 21, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live