Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Mengi wawasili Kilimanjaro, kuzikwa kesho

56226 Pic+mengi

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi umewasili leo, Jumatano, Mei 8, 2019 katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

Ndege namba 5H-PWC ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyokuwa imeubeba mwili wa Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita ya Mei 2,2019 akiwa Dubai, Falme za Kiarabu, imewasili asubuhi hii.

Viongozi mbalimbali wamejitokeza kuupokea mwili wa mfanyabiashara huyo ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho, Alhamisi, kijijini kwake Nkuu, Machame mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya viongozi waliokuwapo uwanjani hapo ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, wakuu wa wilaya za mkoa huo, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na baadhi ya wakuu wa wilaya za mikoa ya kanda ya kaskazini.

Endelea kufuatilia Mwananchi



Chanzo: mwananchi.co.tz