Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigulu akerwa na wabunge kulalamika

Mwigulu Bajetii Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akerwa na michango ya baadhi ya wabunge wanaoeleza tu matatizo bila kutaja suluhisho huku akitaka umakini wa kauli zitolewazo kwa kuwa nchi nyingine huchangia kushusha uchumi.

Aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akifafanua hoja mbalimbali za wabunge zilizotolewa wakati wakichangia taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

“Ninaomba tuelewane vizuri sana, vinginevyo tutabadilisha Bunge hili kuwa eneo la kujadili matukio. Hiki chombo ni kikubwa sana si cha kujadili tu matukio. Kinatakiwa kiishauri serikali namna gani inaweza kuweka mipango yake ya kuwatoa Watanzania kwenye umaskini.

Mwigulu alisema leo kwa sababu inasikika vizuri kwa watu, ukionekana unasemea bei kila mmoja anaiongelea.

“Lakini twendeni kwenye uhalisia, nchi hii ina wazalishaji na walaji, mara zote tukumbuke hili na hivyo vyakula vinavyozalishwa havizalishwi kwa mashamba ya vijiji vya ujamaa, ni watu binafsi wanaingia kuzalisha anajipinda kuzalisha. Wabunge kama watunga sera na sheria lazima wawe makini kuweka uwiano wa hayo maeneo mawili.

“Mtu yupo pale kwenye uzalishaji anasema ‘serikali inajificha tu kwenye Ukraine, sisi tumezalisha hapa, kwa nini bei iko juu? Mmezalisha Mwanzugi lakini Mwanzugi hamtengenezi mbolea, mbolea mliyotumia kuzalishia ni ya bei ya juu ndio ile iliyosababisha yale yatakayozalishwa kama mfuko ulitumia wa Sh. 120,000 ni lazima mazao kijijini kwao yatakuwa na bei ya juu,” alisema.

Waziri huyo alisema ni lazima wanapoeleza matatizo yaliyopo, waeleze na hatua zilizochukuliwa wasionyeshe ufahari katika kuwatajia Watanzania matatizo kwamba kuna bei wakati wananchi wanazijua na kila siku wananunua vitu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti ukiona mara zote kelele zinapigwa kwenye haya mambo ya dharura, kuwa makini sana. Wakati mwingine unaweza kubeba na deal (mambo) ya watu humo humo. Lazima tuwalinde wakulima wetu na lazima tuwalinde walaji wetu,” alisisitiza.

Kuhusu hoja ya akiba kushuka kutoka dola bilioni 6,000 hadi dola bilioni 4,500, Mwigulu alisema masomo ya uchumi ni sayansi.

“Twendeni tufuatilie kwa umakini ilipokuwa 6,300 tulikuwa trilioni moja fedha ilikuwa tumeitoa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), sasa tumeichukua ile tumejengea madarasa yote unategemeaje iwe ile ile.

“Haya ndiyo matatizo ya kuonea huruma mbegu, unaogopa kupanda kwa sababu mbegu itapungua, panda ili uvune zaidi. Pia tuna miradi mikubwa kuliko nchi yoyote ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na vitendea kazi tunavyojengea tunaagiza nje, unategemeaje reserve ziwe zile zile tu.

“Hii ni kazi sana kufundisha mtu yule yule ametaka kwa makusudi kutoelewa, haiwezekani tukawa tunatumia muda wa Bunge kujadili kitu kile kile tunataka kupata nini, hatuna mashaka kuhusu ‘reserve’ (akiba), nchi yetu ipo na zaidi ya miezi minne ya nukta saba importation (agizaji) wastani ni miezi minne tu tuko makini kwenye hilo.

“Hata deni la taifa tuna asilimia 73 ya mikopo yetu tangu uhuru imekopwa kwa concession (makubaliano) ya kipindi cha miaka 10 na kiwango cha riba ni 0.75 ambapo asilimia 26 inayobakia ni commercial (kibiashara) ambayo tumeamua kukopa kwa sababu ni miradi ambayo isingeungwa mkono.

“Tuna uhakika Bwawa la Mwalimu Nyerere litalipa, reli italipa, sasa hapa tunatisha tisha watu nini na kwa ajili ya nini, na sasa niwahakikishe hii si ‘Honorable Doctor’ (udaktari wa heshima) nimeingia darasani.

“Mheshimiwa Rais Samia mbinu alizochukua na maono aliyoyaleta kwenye masuala ya kichumi si yakutilia mashaka wafuatilieni wabobezi wa IMF, WB (Benki ya Dunia) na wachumi wote wanasema ‘uchumi wa Tanzania, uko pazuri na unaelekea pazuri’ .

“Haya si maneno ya Mwigulu, IMF wamesema hivyo, WB wamesema hivyo, tuache kujidharau dharau, Watanzania tumezoea sana kujidharau, hata juzi ilielezwa kwamba timu ya Tanzania ni ya tano, jamaa mmoja anasema haiwezekani ligi yetu iwe ya tano,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: